Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

WALEZI VITUO VYA KULEA WATOTO WAJENGEWA UWEZO KUIJUA PJT_MMMAM

\\
Mwezeshaji wa mafunzo Elizabeth Mweyo kutoka Manispaa ya Shinyanga
Na Stella Herman,Shinyanga
WALEZI na wasimizi wa vituo vya kulea watoto wadogo Mchana (Daycare) Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutambua programu Jumuishi ya  Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM  ili kuwaweka watoto kwenye ukuaji wenye utimilifu.

Hayo yalisemwa jana  na Afisa Ustawi wa Jamii  kutoka Manispaa hiyo  Elizaberth Mweyo ambaye alikuwa mwezeshaji katika semina ya siku mbili  kwa walezi na wasimamizi hao zaidi ya 30  iliyoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la ICS  kwa lengo la kuwajengea uwezo na utambuzi wa programu hiyo kwa umuhumu wake.

Mwenyo alisema katika vituo wapo walezi wapya na wengine wazamani  hivyo wanatakiwa kutambua  PJT-MMMAM  na kuzingatia kundi la watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi minane kwa utafiti uliofanyika watoto hao ubongo wao unaendelea kukua na hata kwenye vituo vya kulea watoto  mnao wenye kuanzia umri wa miaka miwili  hadi minne.

"Katika programu Jumuishi tunaangalia  nguzo tano muhimu ambazo zinamuwezesha mtoto kabla ya kuzaliwa na baada ili kuendelea kukua katika utimilifu wake ambavyo  ni lishe,afya bora,Malezi yenye Mwitikio.Ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama"alisema Mweyo.

Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga  Lyidia Kwesigabo ambaye alikuwa mwezeshaji katika mada ya huduma za ulinzi. na usalama  wa mtoto alisema vipo viashiria vinavyoonyesha mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na kituo lazima kiwe na kamati inayojumuisha wazazi na kisifsnye kazi zaidi ya masaa 12 wala kulaza watoto (boarding) .

Afisa Programu kutoka Shirika la ICS  Lucy Maganga alisema  katika utekelezaji huu wamekuwa waratibu  na kufanya mambo mawili ya kuimarisha mifumo  na uchechemuzi  na vituo vya kulea watoto ni mojawapo ya kujengewa uwezo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Rueben  ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua semina hiyo alisema wanatambua vituo vinapokea watoto wenye umri wa miaka miwili hadi minne na mnawa andaa kiakili na kimwili  na ndiyo maana mnasisitizwa kuwapa lishe bora yenye makundi ya aina tano za vyakula.

Reuben alisisitiza kwenye maeneo ya vituo kuwepo mazingira  safi na salama, maeneo ya kupumzikia, matundu ya vyoo yenye uwiano ,kutambua umuhimu wa chanjo kwa watoto  na kuwaelimisha wazazi ikiwemo vituo kuvisajili kwa mujibu wa sheria,taratibu na miongozo.

Mwenyekiti wa vituo vya kulea watoto mchana  Manispaa ya Shinyanga  Damari Mollel alisema semina hiyo imekuwa ni fursa kwao kuongeza ubora kuleta ufanisi katika vituo kwa walezi na wasimamizi  kwa kuhakikisha watoto wanakua  kwenye hali nzuri.

Daniel Mboto msimamizi wa kituo cha kulea watoto  alisema programu jumuishi  baada ya kutolewa maelezo ya kina ameweza kuielewa  hivyo matarajio ni kwenda kutekeleza kwa vitendo kwa watoto kwa kuzingatia miongozo na misingi ya ukuaji ubongo kwa mtoto.


Kaimu mganga mkuu Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Reuben
Lucy maganga afisa programu kutoka shirika la ICS
Damari  Molles Mwenyekiti wa vituo vya kulea watoto mchana Manispaa ya Shinyanga
                                                   Afisa ustawi  wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lyidia  Kwesigabo







Post a Comment

0 Comments